Vifo vya watoto vingali juu

26 Februari 2014 Imebadilishwa mwisho saa 14:16 GMT

Shirika la watoto Save the Children linasema kuwa licha ya mafanikio katika kumaliza vifo vya watoto wachana duniani, watoto milioni moja hufariki dunia kila mwaka katika siku yao ya kwanza ya maisha.

Katika ripoti mpya ya shirika hilo la misaada kwa watoto linasema vifo vya watoto wachanga vimesalia kuwa moja ya aibu za dunia ya sasa . Hali ya watoto ni mbaya zaidi hasa katika mataifa yanayokabiliwa na mizozo.

Nako nchini Kenya ambapo licha ya serikali kuzindua huduma za bure kwa akinamama wajawazito,idadi ya watoto wanaozaliwa na kufa bado inandelea kuongezeka kama navyosimulia mwandishi wetu Gladys Njoroge