Msanii wa Bongo Ray C
Huwezi kusikiliza tena

Ray C: 'Dawa za kulevya ni hatari'

Katika Misemo ya kale upo msemo usemao aisifuye mvua,imemnyea.

Usemi huu unaweza kufananishwa na kauli ya Msanii maarufu wa Muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Rehema Chalamila almaaruf Ray C,ambaye hivi karibuni alitoa wito kwa serikali kuwanyonga wale wote wanajihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Mwanamuziki huyo hivi sasa yuko kwenye kliniki maalum akipata tiba kutokana na kuathiriwa na matumizi makubwa ya dawa za Kulevya, baada ya kupata msaada kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania.

Erick David Nampesya alikutana naye hivi karibuni jijini Dar es Salaam.