Huwezi kusikiliza tena

Upishi si wanawake tu!

Ali Said Mandhry, kwa jina la umaarufu Chef Ali L'atiste ni mpishi mwenye umri mdogo nchini Kenya.

Amezusha msisimko katika kazi ya upishi na maandalizi, kutokana na mtindo wake wa kutengeneza keki zinazoashiria Afrika.

Akiwa na umri wa miaka 25, amekabiliana na itikadi kwamba, ni wanawake tu, wanaopaswa kuwa jikoni. Kipaji chake kimemfanya kuwa mashuhuri na kutajirika vile vile.

Ametajwa kama mojawapo ya wapishi watano wakuu wa vyakula vya kiafrika. Maryam Dodo Abdalla amekutana naye ametuandalia taarifa ifuatayo...