Huwezi kusikiliza tena

Wakimbizi wa Sudan.K wamiminika Kenya

Huku mapigano yakiendelea Sudan Kusini, mamia ya wakimbizi wanaendelea kuingia nchi jirani ya Kenya.

Kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi (UNHCR), takriban wakimbizi 20,000 wameshaingia Kenya kwa miezi miwili tu.

Wakimbizi hao wamehifadhiwa katika kambi ya Kakuma. Kambi hiyo imekuwa ikiwahifadhi wakimbizi wa Sudan Kusini tangu mwaka wa 1992.

Lakini kama anavyoripoti mwandishi wetu Caroline Karobia aliyezuru kambi hiyo, baadhi yao wamekuwa wakimbizi kwa mara ya pili sasa.