Huwezi kusikiliza tena

Vijana wakumbatia kilimo Kenya

Ukulima kwa muda mrefu imekuwa ni shughuli ambayo vijana wengi hawapendi kuifanya huku wengi wakiiona kama kazi mtu anayoifanya baada ya kusataafu kazi za ofisini.

Hata hivyo nchini Kenya kwa sasa hali ni tofauti kwani vijana wengi wameanza kuipenda kazi hii ambayo wanasema inawawezesha kukidhi mahitaji yao kimaisha kama alivyoshuhudia mwandishi wetu Zainab Deen.