Huwezi kusikiliza tena

Mwaka wa Kifarsi kukaribishwa Iran

Mwaka mpya wa Kifarsi unakaribia kwa haraka na raia wa Iran wanatajitayarisha kuusherehekea kwa hamu.

Mwaka huu, sherehe za 'Nowruz' zinakuja wakati kuna wasiwasi wa kifedha nchini humo hasa kutokana na vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa taifa hilo.

Lakini pia kuna matumaini baada ya hatua muhimu iliyofikiwa katika mazungumzo ya nuklia kati ya Iran na mataifa ya magharibi mwishoni mwaka jana.

kwa mara ya kwanza katika miaka mitano, BBC imepewa kibali kuingia nchini humo. Kassim Kayira anaeleza.