Huwezi kusikiliza tena

Dhiki na mahangaiko nchini Syria

Kwa miaka mitatu sasa, majeshi ya serikali na waasi wanapigana kutaka kudhibiti nchi ya Syria, huku taabu na dhiki kwa mamilioni ya raia ikizidi.

Imekuwa vigumu kusuluhisha mzozo huu kwa juhudi za kidplomasia - kama mazungumzo ya hivi maajuzi mjini Geneva - au kwa vita.

Mzozo huu ulianza kwa maandamano jijini Deraa, kwa wito wa demokrasia zaidi baada ya vuguvugu la nchi za Kiarabu kushuhudia mapinduzi ya kiraia.

Lakini badala yake kukazuka vita vikali vya wenyewe kwa wenyewe.

Inakisiwa kuwa mapigano haya yamewalazimisha Wasyria milioni sita nukta tano kuhama makwao na kuwa wakimbizi wa ndani, huku wengine milioni mbili na nusu wakikimbilia nchi jirani.

Kwa sasa, maisha ya mamilioni ya watu waliolazimika kutoroka yamekuwa vipi katika miaka hii mitatu iliyopita?

Joan Simba anatueleza zaidi.