Huwezi kusikiliza tena

Vita dhidi ya magenge DRC

Katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Kinshasa, polisi wamekuwa wakipambana na magenge ya majambazi mitaani.

Maafisa wa serikali wanasema harakati hizo za polisi zimefanikiwa sana, na vijana waliokuwa wakihusika na mauaji, uporaji mali, na ubakaji, sasa hawaonekani tena.

Lakini mashirika ya kutetea haki za binadamu yanadai vijana wengi wameuawa mikononi mwa polisi. Lubunga Bya'ombe anaarifu zaidi kutoka Kinshasa.