Huwezi kusikiliza tena

Watoto wa Marais wana haki kujiunga na siasa?

Katika mfululizo wa makala kuhusu uhuru leo tunaangalia uhuru katika kufanya shughuli za siasa nchini Tanzania.

Katiba ya nchi hiyo imetoa uhuru kwa mtu yeyote kufanya siasa ikiwa ni pamoja na kugombea nafasi yoyote anayoitaka.

Je raia wote wa nchi hiyo wanatumia uhuru huo kama ulivyotolewa na Katiba ya nchi hiyo

Mwandishi wetu wa BBC mjini Dar es Salaam John Solombi amepata nafasi ya kufanya mahojiano na mtoto wa Rais Jakaya Kikwete , Ridhiwani Kikwete ambaye ni mwanasiasa kijana anafuata nyayo za baba yake.