Huwezi kusikiliza tena

Rais Zuma alitumia pesa za umma

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, ameshutumiwa rasmi, na kwa kauli kali kwa kutumia mamilioni ya dola ya fedha za umma kwa ajili ya kufanya ukarabati wa kiusalama katika jumba lake binafsi.

Taarifa iliyotolewa na tume ya kupambana na ufisadi, iliyowasilishwa na mratibu wa masuala ya umma, imemtuhumu rais Zuma kwa kutofuata maadili.

Uchunguzi huu unafuatia tuhuma kupitia vyombo vya habari vya Afrika Kusini kuwa dola milioni ishirini zilitumika kwa ajili ya vitu vya anasa ikiwemo kujenga bwawa la kuogelea. Alex Mureithi anatuarifu zaidi.