Huwezi kusikiliza tena

Washambuliaji kanisa Kenya wasakwa

Taharuki imetanda katika pwani ya Kenya baada ya watu watano kuuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa na watu waliojihami kwa silaha. Watu hao walifyetua risasi ndani ya kanisa moja katika eneo la Likoni. Polisi katika eneo hilo, wanasema washambuliaji waliingia kwa nguvu kanisani, na kuwafyetulia waumini risasi. Maryam Dodo Abdalla amezungumza na Bozo Jenje, ambaye ni mwandishi habari mjini Mombasa.