Huwezi kusikiliza tena

Wasimulia masaibu chini ya B.Haram

Mashambulio ya kundi la Waislamu la Boko Haram nchini Nigeria yameongezeka katika siku za karibuni kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Zaidi ya watu mia tano wameuawa mwaka huu wakiwemo vijana ishirini na tisa waliovamiwa ndani ya shule ya bweni.

Kundi la Boko Haram limeshambulia misikiti, makanisa na vituo vya kijeshi.

BBC imeweza kukutana na watu kadha walioathirika kutokana na vurugu hizi wakiwemo wasichana waliotekwa na kundi hilo. Kassim Kayira anaeleza zaidi.