Huwezi kusikiliza tena

Wakimbizi Kenya waagizwa kurudi kambini

Serikali ya Kenya imewaagiza wakimbizi wote wanaoishi nje ya kambi za Kakuma na Dadaab kurudi katika kambi hizo haraka iwezekanavyo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watakaokosa kufuata agizo watachukuliwa hatua za kisheria

Halkadhalika imetangaza kusitisha usajili wa wakimbizi zaidi katika maeneo ya mijini ikiwemo Nairobi, Mombasa, Malindi, Isiolo na Nakuru.

Haya ni wakati maafisa mia tano zaidi wa kikosi cha usalama wametumwa katika mji mkuu Nairobi na Mombasa, ambapo watu watano waliuawa walipofyetuliwa risasi wakiwa kanisani na watu waliojihami kwa silaha.

Sikiliza mahojiano kati ya Maryam Dodo Abdalla na msemaji wa waziri wa usalama wa ndani Kenya, Mwenda Njoka.