Huwezi kusikiliza tena

Tisho kwa kilimo cha Mwani Zanzibar

Ukulima wa mwani umekuwa na umuhimu mkubwa katika kuinua uchumi wa Zanzibar, lakini hivi sasa zao hili linaonekana kuwa hatarini kupotea.

Ajira za watu elfu ishirini na tatu, wengi wao wanawake, ziko hatarini. Jitihada za kufahamu nini hasa sababu kuu ya kupotea kwa zao hilo, baadhi ya wataalam wanasema mabadiliko ya tabia nchi huenda ndio chanzo.

Mwandishi wa BBC Aboubakar Famau alitembelea Zanzibar