Huwezi kusikiliza tena

Vita vya Kenya dhidi ya ugaidi

Serikali ya Kenya imeahidi kuendeleza juhudi za kuwawinda magaidi wanaondelea kusababisha usalama mdogo nchini humo.

Hii i,etokea siku moja tu baada ya watu wasiojulikana kulipua bomu lililowaua polisi wawili na watu wengine wawili nje ya kituo cha polisi.

Kenya imekuwa ikikabiliana na mashambulio ya kigaidi hasa yanayofanywa na kundi la Kisomali la Al Shabab. Idara za usalama zilianzisha mikakati ya kuwakamata wanaoshukiwa kuwaunga mkono magaidi hao.

Robert Kiptoo anaarifu zaidi.