Huwezi kusikiliza tena

Mama:'Mimi huwahami wanangu kwa Kondomu'

Jinsi maisha ya sasa yanavyokwenda, wewe kama mzazi unaweza kumpa mtoto wako zawadi gani ambayo daima hatakusahau? Je ni pesa? Hapana.

Na Jee Elimu? Labda! Lakini, mama mmoja mjini Nairobi anaona zawadi kubwa inayowafaa watoto wake na hata wale wa jirani zake ni mipira ya Kondom.

Mwandishi wetu Seif Abdallah alikutana na mama huyo anayesema kuwa anawakinga vijana wake kutokana na maambukizi ya HIV mjini Nairobi.