Huwezi kusikiliza tena

Kauli ya Zitto Kabwe kuhusu katiba TZ

Nchini Tanzania, hivi karibuni kulikuwa na mvutano mkubwa kule Dodoma katika Bunge maalum la Katiba, wakati wa kujadili rasimu ya katiba mpya.

Mijadala ilikuwa mikali kwa zaidi ya siku sitini kabla Bunge hilo maalum halijaahirishwa.

Mmoja wa wajumbe wa Bunge hilo ni Zitto kabwe, yupo hapa London kikazi na nilizungumza naye.

Kwanza nilitaka kujua hawaoni kama hawakuwatendea haki Watanzania kwa kutumia muda na pesa nyingi bila ya kupitisha yale yaliyokuwa yakitarajiwa?