Huwezi kusikiliza tena

Je Rais Museveni atagombea Urais tena?

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema sio juu yake kuamua kuendelea kuwa kiongozi wa nchi hiyo.

Amesema changamoto zinazokabili nchi, ndio zitaamua nani anafaa zaidi kuliongoza taifa hilo lililopata uhuru wake kutoka Uingereza mwaka 1962.

Rais Museveni amesema muda utakapowadia, Uganda itajua inamhitaji nani. Alizungumza na Salim Kikeke na kwanza kumuelezea mwelekeo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.