Huwezi kusikiliza tena

Msingi wa uhusiano mwema

Jimbo la Somaliland mwishoni mwa wiki lilisherehekea miaka 23 ya Uhuru tangu kujitenga na Somalia.

Jimbo hilo limejaribu pasi kufaulu kutambuliwa kama taifa huru na jamii ya kimataifa.

Katika hatua inayowafurahisha viongozi wa eneo hilo, Kenya imetangaza kuwa itafungua afisi ya uhusiano bora kati yake na Somaliland na pia italiruhusu eneo hilo kufungua afisi yake nchini Kenya.

Sikiliza mahojiano kati ya Maryam Dodo Abdalla na Alex Chamwada ambaye ni mwandishi wa Kenya aliyepo katika mji mkuu wa Somaliland, Hergeisa kuhusu maadhimisho hayo.