Huwezi kusikiliza tena

Msanii wa Tanzania asiyevaa viatu

Ni jambo la kawaida kuwaona wasanii wengi wakifanya mambo ambayo ni tofauti na wengine. Mfano wapo ambao huvaa mavazi yenye mishono na mitindo ya ajabu ajabu ili kuwatofautisha na watu wengine.

Lakini unajua yupo msanii nchini Tanzania ambaye yeye ameamua kutovaa kuvaa viatu katika maisha yake yote?

Mwandishi wetu wa Dar es Salaam John Solombi alipata nafasi ya kuzungumza na Msanii huyo Mrisho Mpoto ambaye ni msanii wa muziki wa asili na kwanza alimuuliza ni kwanini aliamua kutovaa viatu katika maisha yake ?