Huwezi kusikiliza tena

Je Joyce Banda atarudi ikulu Malawi?

Wanachi wa Malawi wamepiga kura katika uchaguzi wenye ushindani mkubwa, huku Rais Joyce Banda akichuana na wapinzani wengine kumi na mmoja.

Bi Banda aliingia madarakani miaka miwili iliyopita kufuatia kifo cha ghafla cha Rais Bingu wa Mutharika.

Waandishi wanasema sifa yake imegubikwa na kashfa ya rushwa, ijulukanayo kama 'Cashgate' na kusababisha wahisani kupunguza misaada.

Amekana kuhusika kwa namna yoyote.

Baruan Muhuza anaarifu zaidi