Huwezi kusikiliza tena

Njaa Sudan Kusini inaweza kuzuilika

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Valerie Amos ameonya, kuna uwezekano mdogo wa kuzuia baa la njaa Sudan Kusini.

Akizungumza na BBC katika mkutano wa kimataifa wa wahisani nchini Norway, Baroness Amos amesema usambazaji wa chakula na mbegu ni lazima uwafikie wanaohitaji zaidi, kabla mvua hazijaanza kunyesha.

Na wakati huohuo mashirika ya kutoa Misaada yanaonya Njaa itaikumba Sudan Kusini kwa kiwango kikubwa kuliko vile ilivyotokea Ethiopia miaka ya themanini.

Ukosefu mkubwa wa chakula unatishia maisha ya mamilioni ya watu, ilhali nchi hiyo inakabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe, baina ya majeshi ya serikali na waasi. Mgogoro huo umesabisha kuenea kwa uhasama wa makabila makuu nchini humo, Wa-Dinka na Wa- Nuer, jambo hili limesabaisha mamilioni ya watu kuzikimbia nyumba zao.

Suluma Kassim, na taarifa hiyo.