Huwezi kusikiliza tena

Vijana wa TYSA kuwakilisha Kenya Brazil

Kenya haitakua kwenye kombe la dunia nchini Brazil lakini itawakilishwa nchini humo na vijana wa timu ya Trans Nzoia Sports Association kwa kifupi TYSA.

Timu hii ni miongoni mwa timu 32 zilizochaguliwa na shirikisho linalosimamia kandanda duniani FIFA kushiriki mashindano ya vijana walio chini ya umri wa miaka 18, Football For Hope Festival, yatakayokayofanyika mwezi Julai, na ni mechi za wachezaji watano kila upande ambazo huchezwa bila refa.

Kaunti ya Trans Nzoia iko kilomita 400 kaskazini-magharibi mwa jiji la Nairobi.

Mwandishi wa michezo wa BBC John Nene alitembelea timu hiyo katika makao makuu ya TYSA yaliyoko kijiji cha Makindu, na akatuandalia ripoti ifuatayo…….