Huwezi kusikiliza tena

Wakulima wanavyosumbuka Tanzania

Ukosefu wa soko la uhakika kwa wakulima na miundombinu mibovu ya barabara ni miongoni mwa changamoto kuu zilizojitokeza kwa wakulima huko nchini Tanzania.

Takriban wakulima elfu tisa wametoa kero zao katika kura ya maoni iliyoandaliwa na Redio ya Kimataifa ya Wakulima kwa kupitia njia ya simu.

Lengo la utafiti huo ambao unazinduliwa rasmi hii leo ni kupaza sauti za wakulima ili kero zao zisikike katika ngazi mbalimbali.

Mwandishi wetu Aboubakar Famau ametuandalia taarifa ifuatayo.