Huwezi kusikiliza tena

Taarabu ya ukumbini yakemewa Rwanda

Baraza la waislamu nchini Rwanda limesimamisha shughuli za burudani za akina mama katika kumbi maalum wanapokutana kucheza na kutoa michango ya hali na mali kwa ajili ya vijana wanaojiandaa kufunga ndoa.

Viongozi hao wanasema akina mama wa kiislam wanakiuka sheria za dini kwa kucheza muziki wa taarabu kwa mbwembwe na mitindo isiyofaa.

Kutoka Kigali mwandishi wetu John Gakuba ametuma ripoti hii.