Huwezi kusikiliza tena

Kimya cha dakika moja kwa wandishi

Wandishi wa habari wa BBC waliungana na wenzao kutoka mashirika ya kimataifa ya habari kukaa kimya kwa dakika moja.

Hii ni njia yao ya kupinga hukumu ya kifungo cha miaka saba hadi kumi cha wandishi wa shirika la bahari la Al Jazeera, katika hukumu iliyotolewa Jumatatu na mahakama nchini Misri.

Hatua ya wandishi wa BBC imekuja siku moja baada ya hukumu hiyo kutolewa mjini Cairo.

''Hukumu hii inakwenda kinyume na haki,'' alisema mkuu wa kitengo cah habari cha BBC James Harding.