Huwezi kusikiliza tena

Niqab ni haramu nchini Ufaransa

  • 2 Julai 2014

Mahakama ya haki za binadamu barani Ulaya imeamrisha kuendelea kutekelezwa hukumu ya kupiga marufuku vazi la hijab linalofunika uso mzima nchini Ufaransa.

Kesi hiyo iliwasilishwa na mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka ishirini na nne raia wa Ufaransa ambaye alidai kuwa marufuku hiyo inakiuka haki zake za kuabudu na kujieleza.

Mahakama hiyo hata hivyo imesisitiza kuwa Ufaransa inayo haki ya kuhifadhi utangamano na usawa katika jamii kwa kuweka marufuku hiyo.

Sheria hiyo iliwekwa nchini Ufaransa miaka minne iliyopita na tangu hapo Ubelgiji imeiga.