Huwezi kusikiliza tena

Ziwa Victoria hatari kwa wasichana Tanzania

Idadi kubwa ya wasichana waliopo kando kando ya visiwa vya ziwa Victoria mkoani Mwanza nchini Tanzania, wapo katika hatari ya kuambikizwa virusi vya HIV kutokana na ngono isiyo salama.

Baadhi ya wasichana pia wana hata chini ya umri wa miaka kumi na nane.

Wanawake wengine wamesema wavuvi huwalazimisha kufanya ngono bila kinga.

Mwandishi wa BBC Aboubakar Famau ana taarifa zaidi.