Raila Odinga akizungumzia kura ya maoni Kenya
Huwezi kusikiliza tena

Upinzani wapendekeza Kura ya maoni Kenya

Siku ya Jumatatu maelfu ya wafuasi wa upinzani walikusanyika katika medani ya Uhuru katika mji mkuu wa Kenya Nairobi kulalamikia maswala ambayo wanasema serikali imepuuza kuyatekeleza.

Mkutano huo uliitishwa na kiongozi wa upinzani na aliyekuwa waziri mkuu wa taifa hilo Raila Odinga.

Bwana Odinga anasema kuwa alitaka upinzani uwe na mazungumzo ya kitaifa na serikali kuhusu matatizo yanayoikabili Kenya ikiwemo ongezeko la gharama ya maisha na ukosefu wa usalama na kwa sasa hawataki tena mazungumzo hayo ila wananuia kuandaa kura ya maoni.

Lakini baadhi ya wachambuzi wanasema kuwa wasiwasi wake mkubwa ni kwamba hayupo madarakani baada ya kushindwa katika uchaguzi mkuu uliopita.

Odeo Sirari alizungumza na Bwana Odinga na kwanza akamuuliza ni maswala yapi yatakayoshughulikiwa katika kura hiyo ya maoni wanayopendekeza kama upinzani.