Huwezi kusikiliza tena

Wito wa Malala Nigeria

Mwanaharakati, Malala Yousafzai amekutana na rais Goodluck Jonathan kutaka hatua zaidi kuchukuliwa kuwakoa wasichana waliotekwa na Boko Haram.

Leo ni miezi mitatu tangu wasichana miambili wa shule kutekwa nyara na kundi hilo.

Linataka serikali ibadilishane wasichana hao na wafungwa wa kundi hilo walio katika magereza ya serikalil.

Hii leo Malala amefikisha umri wa miaka 17 na badala ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa aliamua kwenda Nigeria kuishinikiza serikail kuchukua hatua zaidi za kuwaokoa wasichana hao hao.