Huwezi kusikiliza tena

Mkutano wa amani nchini Algeria

Serikali ya Algeria, mnamo Jumatano iliandaa mkutano wa amani ulionuia kumaliza vita Kaskazini mwa Mali.

Mazungumzo hayo yalikuja siku moja baada ya pande zinazozozana kuonyesha ishara nzuri ya kubadilishana wanajeshi na wapiganaji waliokuwa wamezuiliwa.

Wanajeshi 45 wa Mali walikabidhiwa kwa serikali huku waasi 41 wa Tuareg wakiachiliwa huru. Lakini matarajio ya kuwepo amani ya kudumu sio makubwa sana.