Huwezi kusikiliza tena

Masaibu ya watoto wenye HIV Kenya

Mkutano mkubwa zaidi wa weledi na wanaharakati wa ukimwi umeanza mjini Melbourne nchini Australia kujadili jinsi ya kuimarisha mwendo wa kupambana na maradhi hayo.

Mkutano huo unaofanyika mara moja kila miaka miwili uko katika awamu ya ishirini na unafanyika wakati kumepatikana motisha kuwa huenda ugonjwa huo ukathibitiwa katika miaka kumi na mitano ijayo.

Hii leo watu wachache zaidi wanafariki kutokana na ukimwi, ingawaje vikundi kadhaa vya watu vimeachwa nyuma kama vile watoto.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalopambana na ukimwi linakadiria kuwa robo tu ya watoto wanaohitaji dawa za kupunguza makali ya ukimwi wanazipata, na hata wao mara nyingi wanalazimika kutumia dawa za watu wazima kutokana na ukosefu wa zile za watoto.

Mwanahabari wa BBC Anne Soy alitembelea makao ya watoto wanaoishi na virusi vya ukimwi maarufu Nyumbani jijini Nairobi kushuhudia jinsi wanakabiliana na hali hiyo.