Huwezi kusikiliza tena

Afueni kwa wapenzi wa jinsia moja Uganda

Mahakama ya kikatiba nchini Uganda imefutilia mbali sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja ambayo ilisababisha mataifa ya magharibi kuinyima msaada.

Kadhalika sheria hiyo ilizua gumzo sana sio tu Uganda bali kote duniani ambapo mataifa ya Magharibi yalilazimika kuingilia kati.

Inaarifgiwa idadi ya wabunge waliopitishwa mswadaa huo mwezi Februari kabla ya kuidhinishwa kuwa sheria, hawikutosha kupitishwa mswada.

Kwa hilo mahakama ilisema mswada huo ulipitishwa kiharamu

Vitendo vya mapenzi ya jinsia moja, tayari vilikuwa vimeharamishwa Uganda , lakini sheria hiyo mpya pia iliharamisha hatua zozote za kueneza mapenzi ya jinsia moja na wakati huu hata kuwajumuisha wanawake wasagaji kama sehemu ya wapenzi wa jinsia moja.

Mataifa kadhaa ya Magharibi yamesitisha msaada kwa Uganda hasa baada ya sheria hiyo mpya kupitishwa.