Huwezi kusikiliza tena

Wanaume wakimbia tohara Kenya

Nchini Kenya ambapo wanaume kutoka kabila la Turkana na makabila mengine ambayo hayana utamaduni wa kutahiri wanaume sasa wanaishi kwa hofu baada ya baadhi yao kutahiriwa kwa lazima.

Vijana kutoka kabila la Bukusu wamekuwa wakiwavamia wanaume ambao hawajatahiriwa katika mji wa Moi's Bridge na kuwapaka matope na maji taka na kisha kuwatahiri hadharani kando ya barabara .

Wabukusu huchukulia mtu asiyetahiriwa kuwa mchafu na mwoga, lakini wanaume wanaotahiriwa bila ridhaa yao wanalalamika kuwa wanatwikwa utamaduni usio wao.

Odeo Sirari ambaye yupo katika mji huo wa Moi's Bridge amekutana na vijana hao na kutuandalia taarifa ifuatayo.