Huwezi kusikiliza tena

WHO:Ni sawa kutumia dawa za 'Zmapp'

Dawa ambazo bado zinafanyiwa majaribio kutathmini usalama wake kwa binadamu, zinaweza kuwatibu wagonjwa wa Ebola.

Hii ni kwa mujibu wa shirika la afya duniani.

Taarifa hiyo, ilitolewa baada ya wataalamu wa afya kukutana nchini Switzerland Jumatatu, kujadili swala hilo.

Hatua hiyo, imekuja huku Liberia, ikisema kwamba imelazimika kutumia dawa hizo zinazofanyiwa majarabio kuwatibu wagonjwa wa Ebola baada ya ombi lake kwa Marekani.

Shirika la afya duniani linasema kuwa dawa kama hizo zinaweza kutumiwa ila tu lazima pawepo ruhusa na idhini ya kuzitumia.