Kenya inakabiliana na changamoto mpya ya usalama katika vita dhidi ya ugaidi.
Huwezi kusikiliza tena

Alshabab wanasajili wapiganaji Nairobi

Kenya kwa wakati huu inakabiliana na changamoto mpya ya usalama katika vita dhidi ya ugaidi.

Kundi la Al Shabab sasa linalenga Wakenya katika juhudi zake za kuongeza ya idadi ya wafuasi wake.

Baadhi ya walioajiriwa kujiunga na kundi hili tayari wamepelekwa Somalia kwa mafunzo ya kijeshi na sasa wamerudi mitaani Nairobi.

Mwandishi wetu Dennis Okari amekua akifanya uchunguzi kuhusu swala hili katika kitongoji cha Eastleigh mjini Nairobi, kinachokaliwa na Wakenya wenye asili ya Kisomali kiasi kuitwa Mogadishu ndogo.