'Condom' zaagizwa kwa Simu Uganda

13 Agosti 2014 Imebadilishwa mwisho saa 09:21 GMT

Huenda uliwahi kupata huduma ya taxi au kuletewa chakula popote ulipo kwa kupiga tu simu, lakini je utanyanyua simu kwa kutaka huduma ya condom?

Kundi la wafamasia nchini Uganda wameibuka na ubunifu wa kipekee wa kupata huduma ya condomu kwa kupiga tu simu.

Huduma hiyo inaitwa DIAL A CONDOM...yaani unapiga simu tu na kuaguza Condom.

Na hutoa nambari za simu ambazo wateja huweza kupiga, kwa ahadi kuwa watapelekewa aina yoyote ya condom katika kipindi cha dakika 15 au chini ya hapo.

Muliro Telewa anaelezea zaidi kuhusu huduma hiyo.