Afrika Mashariki yaweka mikakati  ya kukabiliana na homa ya Ebola
Huwezi kusikiliza tena

Ebola: Hofu yatanda Afrika Mashariki

Wakuu wa Mamlaka za Usafiri wa Ndege za Raia wanazitaka ndege zinazotua, au hata kupitia, viwanja vya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki - Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda - kuanzisha fomu maalum za kuwafuatilia washukiwa wa Ebola.

Uganda leo imeanza kutekeleza mapendekezo ya usalama kutokana na mkutano wa dharura, mjini Entebbe, wa wakuu wa mamlaka za usafiri wa ndege, Alhamisi iliopita. Alli Mutasa, anaripoti: