Je inawezekana kuwa na kiswahili sanifu kwa mataifa yote ya Afrika mashariki?’
Huwezi kusikiliza tena

Je inawezekana kuwa na kiswahili sanifu?

Image caption Je inawezekana kuwa na kiswahili sanifu kwa mataifa yote ya Afrika mashariki?’

Zaidi ya wanafunzi 500 wa Kiswahili kutoka vyuo vikuu vya mataifa ya Afrika Mashariki Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi wamekusanyika katika Chuo Kikuu cha Laikipia, nchini Kenya kushiriki katika kongamano la siku tatu ambalo huandaliwa kila mwaka kujadili mbinu za kisasa za kuimarisha na kukuza lugha ya Kiswahili.

Kauli mbiu ya kongamano la mwaka huu ambalo limeandaliwa na Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili wa Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki (CHAWAKAMA) ni "Kiswahili Malighafi ya Umoja wa Afrika Mashariki".

Mwandishi wetu Muliro Telewa amehudhuria mojawapo ya vikao vya kongamano hilo na kuzungumza na Shiella Simwa, ambaye ni mhadhiri wa kiswahili katika Chuo Kikuu cha Laikipia Kenya, mlezi wa CHAWAKAMA, Mariam Khamis Masoud, ambaye ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Elimu Chukwani Zanzibar; Ajira Sumaya ambaye ni mwanafunzi wa Chuo cha Walimu, Wilayani Kabale, nchini Uganda; na Ahmed Jumbe Abdallah, Katibu Mkuu wa Chawakama na ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro Tanzania Bara.

Hapa anaanza Ajira Sumaya.