Huwezi kusikiliza tena

Polisi wakana mauaji ya wakazi Tanzania

Jeshi la Polisi nchini Tanzania limekanusha madai ya ukiukaji haki za binadamu pamoja na mauaji dhidi ya wakazi wa eneo la Nyamongo linalozunguka mgodi wa machimbo ya dhahabu wa North Mara ulioko Wilayani Tarime mkoani Mara.

Katika Ripoti iliyotolewa hivi karibuni kwenye Bunge la Uingereza na Wanaharakati wa masuala ya madini, polisi kwa kushirikiana na kampuni ya African Barrick inayomiliki mgodi wa North Mara walishutumiwa kwa vitendo vya mauaji na ukatili dhidi ya wananchi waishio jirani na mgodi huo.

Erick David Nampesya alitembelea eneo la Nyamongo kwenye mgodi huo.