4 hatiani kwa jaribio la kumuua Nyamwasa
Huwezi kusikiliza tena

4 hatiani kwa jaribio la kumuua Nyamwasa

Watuhumiwa wanne waliokuwa wakishutumiwa kujaribu kumuua generali wa zamani wa jeshi la Rwanda Kayumba Nyamwasa wamepatikana na hatia ya kujaribu kutekeleza mauaji na mahakama ya Afrika Kusini .

Wengine wawili wameondolewa mashtaka hayo na kuachiliwa huru .

Kayumba Nyamwasa alitoroka kutoka Rwanda mnamo mwaka 2010 na kwenda Afrika kusini baada ya kutofautiana na rais Paul Kagame na amekuwa akiwashutumu washukiwa wa mauaji yake kushirikiana na Maafisa wa Rwanda.