Huwezi kusikiliza tena

Mwanamuziki hodari wa Kenya apofuka

Je unamkumbuka mwanamuziki hodari wa Kenya Teddy Kalanda na bendi yake ya Them Mushrooms?

Alivuma sana miaka ya tisini kupitia kwa muziki wake na kilichomvumisha ni kuwa muziki wake ulikuwa wa kuwakaribisha watalii nchini Kenya.

Kumbuka nyimbo kama Jambo Bwana, ambapo ziliipatia Kenya sifa kwa watu wa nje? ulikuwa utunzi wa bwana Teddy Kalanda na bendi yake ya Them Mushrooms.

Baada ya miaka mingi katika sanaa ya muziki, Teddy amepoteza kabisa uwezo wa kuona. Hali hii imempata baada ya kufanyiwa upasuaji kadhaa kuanzia mwaka wa 2009.

Licha ya kutoona Teddy ametunga wimbo mpya uitwao KENYA HATUTAKI MATATA ambao bado hajaurekodi na bendi yake ya nyumbani kwao Kaloleni eneo la pwani iitwayo Big Matata .

Anatumia bendi hiyo kukuza vipaji vya vijana.

John Nene amemtembelea Teddy nyumbani kwao Kaloleni na kutuandalia ripoti hii……