Huwezi kusikiliza tena

Mabuu wanavyotumiwa kwa matibabu Kenya

Je unafahamu Mabuu ? Wadudu wanaotokeza mara nyingi katika nyama zinazo oza na sehemu za uchafu na mifereji ya maji machafu?

Basi nisikushangaze sasa ukisikia utaweza kuwakuta katika sehemu nadhifu kama vile mahospitalini. Katika karne za zamani kidogo mabuu hao walikuwa wanatumika kutibu magonjwa hasa sehemu za vidonda, tiba ijulikanayo kama Maggot therapy.

Hata hivyo katika karne iliyopita madaktari walivumbua dawa ya penicilin na wakaachana na mabuu hao.

Lakini sasa mabuu hayo yameanza tena kurejeshwa katika mahospitali kama tiba inayopata umaarufu zaidi kwa vidonda sugu hasa katika nchi kama vile Marekani na Uingereza.

Na kama anavyotuarifu mwandishi wetuAnne Siy, Huenda na Kenya pia wakaanza kuwa maarufu kwa tiba.