Huwezi kusikiliza tena

Zaidi ya 1,900 wamekufa na Ebola

Zaidi ya watu 1,900 wanakisiwa kufariki kutokana na mlipuko wa Ebola katika kanda ya Afrika Magharibi.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO.

Visa 3,500 vimethibitishwa vya watu kuambukizwa ugonjwa huo nchini Guinea, Sierra Leone na Liberia.

''Inakuwa vigumu kudhibiti ugonjwa huo katika mataifa haya, '' alisema mkuu wa shirika hilo Margaret Chan.