Huwezi kusikiliza tena

Glasgow kabla ya michezo ya madola

Kabla ya michezo ya Jumuiya ya madola kuanza mjini Galsgow, Scotland,mwezi jana, maandalizi yalionekana kuwa ya hali ya juu ili washiriki wajisikie wako nyumbani michezo yenyewe ilipoanza.

Michezo hio hufanyika kila mwaka miongoni mwa mataifa yaliyotawaliwa na Uingereza.

Mara ya mwisho ilipofanyika Scotland mwaka 86 nchi za Afrika ziliisusia michezo hiyo kutokana na hatua ya Waziri Mkuu wa Uingereza wakati huo Bi Margaret Thatcher kukataa kuiwekea vikwazo vya kiuchumi serikali ya kibaguzi ya Afrika kusini, sawa na mataifa mengine.

Peter Musembi alikuwepo mjini Glasgow kabla hata ya michezo yenyewe kuanza.