Huwezi kusikiliza tena

Watu mashuhuri walaani udukuzi

Imekuwa wiki ya kufichuliwa kwa watu mashuhuri wenye akaunti za iCloud. Akaunti zingine zilidukuliwa na picha za kibinafsi kuchapishwa kwenye mitandao. Apple inasema kuwa wadukukuzi walifanikiwa kupata majina ya siri ya wenye akauinti hizo. Apple ilisema kuwa hakuna ushahidi wa ukiukaji wa mifumo yake ya usalama. Shirika la FBI sasa linashughulikia kesi hiyo.