Huwezi kusikiliza tena

Mbioni kupambana na njaa Sudan.K

Haijatimu hata miaka minne tangu Sudan Kusini ilipojitenga na Sudan, lakini watu wanaotoa misaada wako mbioni kujaribu kuepusha janga kubwa la njaa.

Umoja wa mataifa umeonya kuwa hali inayoikabili Sudan Kusini inaweza kuwa mbaya kuwahi kuonekana Afrika katika kipindi cha miaka 30.

Umoja huo unasema kufikia mwishoni mwa mwaka huu huenda watu milioni nne wakakabiliwa na njaa kali, na huenda watoto elfu 50 wakaathirika. Mwandishi wetu Emmanuel Igunza ametuma taarifa ifuatayo.