Huwezi kusikiliza tena

Afrika haiwatunzi wazee vyema

Tarehe moja kila Oktoba kila mwaka huwa siku ya kimataifa maalum ya wazee.

Utafiti mpya umeonyesha kuwa Afrika ni moja ya maeneo ambayo maisha ya wazee ni magumu sana na bara ambalo haliwatunzi wazee wake vizuri hasa wale wanaoishi hadi kuwa miaka 60.

Utafiti huo ulichapishwa na shirika la Hepage Iternational baada ya uchunguzi wao katika mataifa 96. Utafiti huo ulizingatia kipato, afya na mazingira wanamoishi wazee hao.

Norway ndio nchi inyowajali zaidi wazee ikifuatiwa na Sweden na Switzerland mtawalia.