Huwezi kusikiliza tena

CUF chapinga rasimu ya katiba TZ

Chama cha Wananchi CUF jana kimefanya mkutano mkubwa wa hadhara huko Zanzibar kuipinga katiba inayopendekezwa ya Tanzania iliyopitishwa na Bunge Maalum.

Huku Wazanzibari wakiwa wamegawanyika, Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF, Maalim Seif Shariff Hamad, amesema rasimu hiyo itaangushwa Zanzibar kama itapigiwa kura ya maoni na wananchi.

Msimamo huo unaonyesha ugumu uliopo katika kukamilisha katiba mpya ya Tanzania ambayo tayari imezongwa na utata wa baadhi ya vyama vya upinzania kuisusia.

Mwandishi wa BBC Hassan Mhelela anasimulia kutoka Zanzibar.