Huwezi kusikiliza tena

Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere

Wananchi wa Tanzania leo wanaadhimisha kumbukumbu ya miaka 15 tangu kufariki kwa Rais wa kwanza na Baba wa Taifa hilo marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mwalimu alifariki nchini Uingereza alikokuwa amaelazwa kwa kusumbuliwa na maradhi ya kansa ya damu.

Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza alitembelea kijijini Mwitongo Butiama Kaskazini mwa Tanzania ambapo amezikwa Kiongozi huyo wa zamani.